Main Menu

Thursday, January 30, 2014

TAARIFA ZA USAJILI ULAYA HIZI HAPA
















Manchester city wamepeleka bid ya paund million 38 kwa ajili ya beki wa fc porto eliaquim mangala


kipa wa Espanyol Kiko Casilla , 27 yupo katika orodha ya makipa wanaowaniwa na  Manchester United, akiwemo pia kipa wa  Leicester City Kasper Schmeichel .

 
meneja wa AS Roma Rudi Garcia amesema hana mpango wa kumuuza kiungo  Miralem Pjanic, kwa  mabingwa wa ufaransa Paris St- Germain.


Newcastle wanajitihidi kumtafuta mbadala wa yohan cabaye anayetimkia psg kutaka kumsajili  kiungo wa Lyon Clement Grenier anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 20 pamoja na Luuk de Jong wa Borussia Monchengladbach


Liverpool baada ya kumkosa salah wametuma bid ya paundi milioni 15  kwa ajili ya winga wa timu ya Dnipro, Yevhen Konoplyanka .

Juventus inafuatilia hali ya nahodha na beki wa kati wa Manchester United Nemanja Vidic , ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni .


Arsenal na Liverpool kwa pamoja wanamfuatilia kinda wa barca Isaac Cuenca aliyeanza mazoezi baada ya kutoka kwenye majeruhi. 

 
Borussia Dortmund wanajipanga kumsajili mshambuliaji manchester united raia wa Javier Hernandez na mshambuliaji wa Manchester City Edin Džeko kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski , ambaye atajiunga na Bayern majira ya joto.

Tottenham inaelekea kukamilish deal la kumsajili mshambuliaji Dimitar Berbatov kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili siku ya ijumaa mpango utakaomuhusisha Lewis Holtby ambaye atahamia Fulham kwa mkopo .

0 comments:

Post a Comment