Main Menu

Wednesday, January 8, 2014

MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA YABADILISHWA MUDA, SASA KUCHEZWA MSIMU WA BARIDI


Baada ya utafiti wa muda mrefu na majadiliano yaliyochukua zaidi ya mwaka mmoja shirikisho la soka ulimwenguni limefikia uamuzi wa kutofanyika kwa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 katika kipindi cha msimu wa kiangazi .

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke michezo ya kombe la dunia haiwezi kufanyika kwa msimu huo nchini Qatar kutokana na hali ya hewa kuwa joto kali na hivyo kuhatarisha afya na usalama wa wachezaji.
Kwa muda mrefu FIFA imekuwa ikifanya utafiti kufuatia malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya mataifa kuhusiana na ugumu wa michezo ya kombe la dunia kufanyika nchini Qatar wakati wa msimu wa kiangazi ambapo hali ya hewa ni nyuzi joto 38 mpaka 40 mazingira ambayo hayawezi kutumika kwa mechi za soka hasa kwa timu za ulaya .
FIFA imetangaza kuwa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 yatafanyika kati ya Novemba tarehe 15 na January 15 katika wakati ambao msimu utakuwa wa baridi.

Maamuzi haya yatazua utata miongoni mwa wadau na wadhamini wa Mashindano haya ikiwemo kampuni ya Fox Sports ya Marekani ambayo imeingia mkataba na FIFA wa kurusha matangazo ya michezo ya kombe la dunia katika msimu wa joto huku wakiwa na mikataba ya kurusha matangazo ya michezo mingine katika msimu wa baridi.

Na ikumbukwe pia qatar ilikua tayari kujenga viwanja ambavyo ingeviwekea vinyonyozi ndani na katika mitaa ya miji ambapo michezo hiyo ingepigwa hali ambayo ingewasaidia wachezaji na watazamaji kukabiliana na hali ya joto. 
       QATAR 5

0 comments:

Post a Comment