Main Menu

Wednesday, January 8, 2014

WACHEZA SOKA MAARUFU WAENDELEA KUJITANGAZA KUWA MASHOGA, JE WATAKA KUMFAHAMU ...? HUYU HAPA.


 Nyota wa zamani wa Ujerumani Thomas Hitzlsperger aliyeanzia soka lake kwenye klabu ya Bayern Munich  amejitangaza kuwa shoga .

Nyota huyo aliwahi kucheza kwenye ligi ya England kwa muda wa miaka mitano akicheza kwenye klabu ya Aston Villa kabla ya kujiunga na VFL Stutgart ya nyumbani kwao ujerumani ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya Ujerumani Bundesliga.


Thomas pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambako alicheza mechi zote za hatua ya mtoano kuanzia robo fainali , nusu fainali na fainali.
 
Kiungo huyu mshambuliaji pamoja na kuwa raia wa Ujerumani alichea sehemu kubwa ya soka lake nchini England kwenye timu za Aston Villa, West Ham United na Everton pamoja na Stuttgart, Bayern Munich alikoanzia soka lake na Werder Bremen. 

Moja ya vitu ambavyo Hitzlsperger atakumbukwa navyo ni mashuti makali aliyokuwa anapiga kwa mguu wake wa kushoto na alifunga mabao mengi sana kwa style hiyo.

Kiungo huyu alistaafu kucheza soka mwaka jana akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuandamwa na majeraha tofauti ya goti kwa muda mrefu.

Thomas Hitzlsperger anakuwa mchezaji wa pili maarufu kujitangaza kuwa shoga baada ya mchezaji wa zamani wa Leeds United Robbie Rogers ambaye kwa sasa anacheza kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy naye kujitangaza kuwa shoga.

0 comments:

Post a Comment