Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa mipira kumi kwa kila chama cha
mpira wa miguu cha mkoa ili isaidie kuendesha ligi za mikoa husika.
Mipira
hiyo 250 yenye thamani ya sh. 16,250,000 tayari imeanza kutumwa kwa
makatibu wa vyama vya mikoa husika. Mpira mmoja una thamani y ash.
65,000.
Ni maratajio ya TFF kuwa mipira hiyo itakuwa chachu kwa vyama vya mikoa katika uendeshaji wa ligi hizo.
MITIHANI YA WAAMUZI KUFANYIKA JUMAPILI
Robo
ya mwisho ya mitihani ya waamuzi (Cooper Test) na utimamu wa mwili
(physical fitness test) kwa mwaka 2013 kwa waamuzi inafanyika Jumapili
(Desemba 15 mwaka huu).
Mitihani
hiyo inayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam inashirikisha waamuzi
wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) na wale wa
kundi la waamuzi (elite) ambao wanaweza kupendekezwa kupewa beji za
FIFA.
Wakufunzi wa mitihani hiyo ya waamuzi ni Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
Waamuzi
wa FIFA watakaofanya mitihani hiyo ni Ferdinand Chacha, Hamis
Chang’walu, Israel Mujuni, Jesse Erasmus, John Kanyenye, Josephat
Bulali, Mgaza Kinduli, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Samwel Mpenzu na
Waziri Sheha.
Washiriki
kutoka kundi la elite ni Charles Simon, Dalali Jaffari, Hellen Mduma,
Issa Bulali, Issa Vuai, Janeth Balama, Jonesia Rukyaa, Judith Gamba,
Lulu Mushi, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Mohamed Mkono.
KILIMANJARO STARS YAREJEA DAR
Timu
ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la
Chalenji iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es
Salaam leo.
Kilimanjaro
Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jioni kwa
ndege ya RwandAir.
Wenyeji
Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada
ya kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana
Uwanja wa Nyayo.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment