Main Menu

Wednesday, December 25, 2013

MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA


 Mtangazaji wa kipindi cha mboni show Mboni Masimba akimkabidhi zawadi mtoto yatima Ally Mustapha baada ya kuimba vizuri katika mlo uliandaliwa na Mboni katika ukumbi wa Highland hall
 baadhi ya watoto yatima wakiwa katika ukumbi wa highland hall  na mc wa shughuli hiyo Mc Zipompampa akiwa na mtoto Ally Mustapha.
 Wageni rasmi katika hafla maalum ya mlo wa pamoja uliondaliwa na kipindi cha Mboni Show, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi (kulia), Mboni Masimba katikati akiwa na mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Asas Abri, mgeni kutoka Nigeria.

=======  ======  =======


MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV,Mboni Masimba jana amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.

Katika hafla hiyo umejumuisha vituo vitatu vya watoto yatima vilivyoko mkoani Iringa vya Upendo center na Tosamaganga na kingine kilichoko katika wilaya ya Mufindi cha Moyo kwa Moyo.

Hafla  hiyo  ya  kula  chakula cha mchana na yatima  imefanyika katika ukumbi wa Highland hall na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara maarufu mkoani hapa akiwemo mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Abri Asas na mgeni rasmi alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi..

Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha  kipindi chake cha Mboni Show  kwa kujumuika na watoto hao.
.

Na Denis Mlowe.

0 comments:

Post a Comment