Main Menu

Wednesday, December 25, 2013

LUKUVI AWATAKA WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA AMANI,UTULIVU NA UPENDO, CHEKI PICHA ZAIDI ZA TAMASHA LA CHRISMASS UWANJA WA TAIFA


 Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akizungumza mbele ya watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.Lukuvi amewataka watazamaji na washabiki wa tamasha hilo  na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwa amani,upendo na utulivu,ameongeza kuwa pia Serikali itahakikisha usalama upo na wa kutosha kwa watu wake,pichani kati ni Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha hilo Bwa.Alex Msama.
 Mmoja wa wageni waalikwa katika tamasha la Krisimasi,Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pichani kati akiwatakia heri na fanaka Watazamaji na Watazania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya. 
 Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili Upendo Nkone akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo mbele ya mashabiki kibao (hawapo pichani) wakati wa tamasha la krisimasi likiendelea jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini Dar.

 Baadhi ya Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka kikundi cha Living Waters wakitumbuiza kwenye tamasha la Krisimasi lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa,jijini dar.
 Pichani shoto ni Mwimbaji nyota wa muziki wa injili,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima,wakishambulia kwa namna ya pekee kabisa,huku miluzi na shangwe za watazamaji zikivuma kila kona ya uwanja kwenye tamasha la krisimasi.
 Rose Muhando akiimba wimbo wake wa Utamu kwa Yesu mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani)  ndani ya uwanja wa Taifa.

 Baadhi ya Waimbaji wa kundi la Glorious wakiimba jukwaani
Mwimbaji wa nyimbo za injili,Boni Mwaitege pichani kati na madansa wake wakiwaimbisha mashabiki wao jioni ya jana.
 Sehemu ya umati wa Watu wakifuatilia tamasha la Krismasi, ambalo limejumuisha wanamuziki mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.


0 comments:

Post a Comment