Main Menu

Sunday, December 15, 2013

BREAKING NEWS; MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA AUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI MCHANA HUU

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini mwanza. 

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani.? Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani.

Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia m1 kwa risasi ndipo wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na kila dhana ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji yametokea mchana huu majira ya saa 7.

Kamanda wa polisi Mwanza amethibitisha japo hajasema nini chanzo cha mauaji.

chanzo jamiiforum

0 comments:

Post a Comment