Main Menu

Tuesday, August 6, 2013

MBAKAJI WATOTO 11 ALIYEACHILIWA HURU NCHINI MOROCCO, KUHUKUMIWA NCHINI HISPANIA

Maafisa nchini Uhispania wamemkamata mwanamume anayetuhumiwa kuwanajisi watoto 11 walio kati ya umri wa miaka 4 na 15 nchini Morocco aliyeachiliwa hivi karibu baada ya kusamehewa na mfalme wa Morocco.


Daniel Galvan Vina anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama kuu nchini Uhispania hii leo.


Vina alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 kabla ya mfalme Mohammed wa sita kumsamehe pamoja na wafungwa wengine 48 raia wa Uhispania wiki iliyopita.


Taarifa za kuachiliwa kwake zilizua maandamano makubwa yaliyoambatana na ghasia nchini Morocco na kumlazimu mfalme huyo kubatilisha uamuzi wake.


Inasemekana mfalme Mohammed  hakufahamu ukubwa wa kosa alilofanya raia huyo mhispania wakati akitoa amri hiyo ya kumsamehe yeye pamoja na wenzake.

na dwswahili

0 comments:

Post a Comment