Kiasi watu 50,000 waliohudhuria kumbukumbu hiyo walikaa kimya kwa dakika moja kutowa heshima kwa maelfu ya watu waliouwawa katika tukio hilo la kihistoria lililoshuhudiwa mwaka 1945 siku kama ya leo.

Mashambulio mengine ya silaha ya bomu la Nuklia yalishuhudiwa siku tatu baadae katika eneo la Nagasaki nchini humo katika mwaka huohuo ambapo maelfu ya wajapan zaidi waliuwawa hatua iliyoichochea nchi hiyo kusalimu amri katika vita vya pili vya dunia.
Waziri mkuu Shinzo Abe akiwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria kumbukumbu hizo amesema nchi yake kama mhanga pekee wa shambulio la bomu la Nuklia,ina jukumu la kutafuta njia za kumaliza uwepo wa silaha hizo.
NA dwswahili
0 comments:
Post a Comment