Jaji Mkuu wa Misri Adly Mansour amepaishwa kuwa
rais wa mpito wa nchi hiyo leo hii siku moja baada ya
kupinduliwa kwa Rais Mohamed Mursi kufuatia
maandamano makubwa ya umma.
Katika hafla
iliofanyika kwenye makao ya Mahakama ya Katiba
amekula kiapo cha kuitumikia serikali ya Jamhuri
kwa kusema kwamba ataheshimu katiba na sheria
na kulinda maslahi ya wananchi.
Mkuu wa majeshi
ya Misri hapo jana alitangaza kuondolewa
madarakani kwa Rais wa nchi hiyo, Mohamed Mursi.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia televisheni, Jenerali
Abdul Fattah al-Sisi pia amesema katiba ya nchi hiyo
imesitishwa.
Msemaji wa chama cha Udugu wa Kiislamu
amesema Mursi yuko katika kifungo cha nyumbani
kwenye makaazi ya rais ambako amekuwa akiishi.
Kuondolewa kwake kunafuatia siku nne za
maandamano ya umma ambapo maelfu ya watu
walikusanyika katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo
kudai kujiuzulu kwa kiongozi huyo.
Jeshi hapo awali
lilimpa rais huyo wa zamani saa 48 kuzungumza na
wapinzani kutafuta usuluhishi wa mzozo wao
venginevyo jeshi litaingilia kati.
Jenerali al-Sisi
alilihutubia taifa baada ya kumalizika kwa muda huo
wa mwisho aliopewa Mursi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment