Maandamano yakiingia uwanjani mwembetogwa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Letisia wWrioba akikagua mabanda mbalimbali katika uwanja huo
Mkuu wa wilaya Dr Warioba akizima moto baada ya kutembelea gari la zima moto
Mchungaji Peter Msigwa akizungumza na wananchi na wakuu wa idara za manispaa ya Iringa
Wakati
maadhimisho ya serikali za mitaa yakifanyika leo, Wananchi wametakiwa kutoziogopa ofisi za manispaa kwa ajili ya kuhoji
masuala ya maendeleo, sanjari na kusoma rasimu ya katiba mpya na kutoa maoni .
Akiwahutubia
wananchi na watumishi wa idara mbalimbali za manispaa ya Iringa, Mgeni rasmi
katika maadhimisho ya serikali za Mitaa, mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Letisia
Warioba mbali ya kuwaagiza waandaaji wa maadhimisho hayo kuwaalika viongozi wa
ngazi za chini katika maadhimisho yajayo, ametoa wito kwa wananchi kutoa maoni ya katiba
mpya kupitia mabaraza ya katiba.
Akisoma taarifa
ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za halmashauri ya Manispaa ya Iringa kaimu
mkurugenzi Imaculeti Senje, amesema ugonjwa wa malaria umeendelea kuongoza kwa
vifo manispaa ya Iringa.
Kwa upande
wake mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa amewataka wananchi
wa manispaa hiyo kutoziogopa ofisi za manispaa na badala yake wajitokeze kuhoji
na kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayowakabili.
Maanzimisho
hayo kwa manispaa ya iringa yamefanyika katika viwanja vya mwembetogwa wakati
ya kitaifa yamefanyika mkoani morogoro wakiwa na kauli mbiu isemayo ‘AMAN,
UADILIFU KWA WOTE NI NYENZO MUHIMU KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA USTAWI WA
SERIKALI ZA MITAA’.
0 comments:
Post a Comment