Main Menu

Tuesday, July 9, 2013

LUIS SUAREZ AENDELEA KUIPA WAKATI MGUMU LIVERPOOL, ATAKA KUCHEZA UEFA.

Wakala wa mshambulizi matata wa Liverpool, Luis Suarez, amefanya mazungumzo na kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers na mkurugenzi mkuu Ian Ayre na kukariri kuwa mchezaji huyo kutoka Uruguay, angali ana nia kubwa ya kushiriki katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao. 


Pere Guardiola alisafiri hadi uwanja wa Mesrseyside na kufanya mazungumzo na wawili hao, baada ya Liverpool kusisitiza msimamo wao wa awali kuwa hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na sita.


Suarez, kwa sasa yuko likizoni, baada ya kuichezea timu ya taifa ya Uruguay, wakati wa michuano ya kuwania kombe la Shirikisho nchini Brazil.


Lakini katika miezi ya hivi karibu, Suarez amedokeza kuwa nia yake kuu msimu ujao ni kushiriki katika michauno ya Ulaya na inaaminika kuwa wakala wake Pere Guardiola alisasilisha ujumbe huo kwa wasimamizi wa klabuhiyo ya Liverpool hiyo jana.

Je ndoto ya Suarez itatimia?

Tayari Liverpool, imekataa ombi kutoka kwa klabu ya Arsenal ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni thelathini, licha ya kuwa mchezaji huyo ameelezea wazi wazi kutoridhishwa kwake na maisha ya Uingereza.
Brendan Rodgers

Kocha wa Liverpool Brenda Rodgers vile vile ameshikilia uzi huo huo wa bodi ya wakurugezi kuwa Suarez haendi kokote. 


Suarez anatumikia adhabu ya kutoshiriki katika mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya  kumuuma mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic wakati wa mechi yao katika uwanja wa Anfeld msimu uliopita na katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na klabu ya Real Madrid. 


Ripoti zinasema huenda Liverpool, ikakubali ombi kutoka kwa klabu ambayo itakuwa tayari kulipia takriban pauni milioni hamsini, sawa na kiasi ambacho Chelsea kililipa wakati ilipomsajili Fernando Torres Janauri mwaka wa 2011.


Msimu uliopita, Suarez alishutumiwa sana, kutokana na kile wakosoaji wake walitaja kuwa mtindo wa kujiangusha ili kupata mkwaju wa adhabu

Chanzo bbcswahili

0 comments:

Post a Comment