Main Menu

Monday, June 24, 2013

SOGGY DOGGY AFUATA NYAYO ZA SUGU, AMUWASHIA TAA NYEKUNDU MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA JIJINI DAR



Wakati watanzania wakiisubiri katika mpya itoe muongozo wa namna ya uundaji na upatikanaji wa wabunge, mkongwe mwingine wa muziki wa kizazi kipya nchini Anselm Tryphone Ngaiza aka Chief Rumanyika aka Soggy Doggy Hunter amemuwashia taa nyekundu mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam kwa madai yakutaka kuchukua nafasi yake kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, mwaka 2015.

Kupitia ukurasa wake wa facebook na tweeter mkongwe huyo amefunguka ifuatavyo  "Shikamoo Mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga, imetosha sasa nadhani ni zamu yangu kuwatumikia wana-segerea 2015 kupitia CHADEMA".
 
Nikipiga nae story asbh ya leo mkongwe huyo ambaye kwa hivi sasa ni mtangazaji wa radio ebony fm ya mkoani iringa amesema pamoja na kutuma ujumbe huo bado hajatangaza nia rasmi, ameongeza kwa kusema kuwa wikiendi ijayo inaweza kuwa na picha rasmi ya kile alichoandika kwenye mitandao ya kijamii.


Hatua ya Soggy ni muendelezo wa msururu wa wanamuziki kuingia kwenye siasa baada ya kufunguliwa njia na Joseph Mbilinyi aka Sugu ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Mbeya mjini, mapema mwezi uliopita mkali mwingine Joseph Haule aka Prof Jay alichukua kadi ya uanachama wa CHADEMA na sasa ni zamu ya Soggy.
 
hapa soggy akisakata kwaito na wafanyakazi wenzake wa ebony fm

Pia wapo wananmuziki waliojiingiza kwenye siasa kama Kala Pina aliyegombea nafasi ya udiwani katika uchaguzi wa mwaka 2010 kupitia CUF, huku mkongwe wa bongo fleva kutoka Morogoro Afande Sele akitajwa kujiunga na moja ya chama cha siasa ambacho akijawekwa wazi na kugombea mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment