Main Menu

Saturday, May 25, 2013

UKOSEFU WA VIFAA NA MASLAHI DUNI KWA ASKARI WA PORINI, WAHATARISHA MISITU NCHINI

                          Sehemu ya uharibifu wa msitu
  Mratibu wa MJUMITA kanda ya nyanda za juu kusini Remmy Lema akiwa na meneja mradi kutoka shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania Elinas Monga wakikagua msitu katika kata ya Migori


  Mwandishi wa habari wa Itv mkoani Iringa Mkumbata akiwa amekusanya matunda aina ya ubuyu yanayopatikana msitu wa nyang'oro kaskazini
                            Moja kati ya miti iliyoharibiwa kwa mashine
                                Hali ni mbaya katika misitu yetu
   Waandishi wa habari, viongozi wa mjumita na Tfcg pamoja na uongozi wa kijiji cha migori wakiwa katika ziara ya ukaguzi wa uharibifu wa misitu
   Afisa mtendaji wa kijiji cha migori Mathayo Michaeli akimuelekeza mratibu wa Mjumita Remmy Lema namna uharibifu unavyofanywa
                    Hali halisi ya uharibifu katika msitu wa nyang'oro
Kiongozi wa askari wa porini katika msitu wa nyang'oro kaskazini uliopo katika kata ya migori wilaya ya iringa akielezea uharibifu unaofanywa na wavamizi wa misitu


Siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuzindua  kampeni ya ufanyaji usafi na utunzaji mazingira nyanda za juu kusini inayoendeshwa na Ebony Fm mkoani Iringa, Ukosefu wa vifaa na maslahi mazuri  kwa askari wa porini, uenda ukasababisha kutoweka kwa misitu  asili nchini, kutokana na kukithiri kwa uvamizi katika misitu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati walipofanya ziara katika msitu wa nyang’oro kaskazini uliopo kijiji cha migori wilaya ya iringa, Ziara iliyofadhiliwa na MJUMITA, kiongozi wa askari wa porini Beatus Kigomba amesema ukosefu wa vifaa na maslahi duni kwa walinzi hao kumesababisha kushindwa kuwadhibiti wavamizi wa misitu.


Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Migori Mathayo Michael amesema uvamizi katika misitu umeongezeka kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika bwawa la Mtera na hivyo kusababisha vijana wengi kutumia misitu kwa ajili ya kujipatia kipato.


Kwa upande wake mratibu wa Mtandao Wa Jamii Wa Usimamizi Wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kanda ya nyanda za juu kusini Remmy Lema amesema kazi kubwa wanayoifanya ni kuwawezesha wananchi kuzifahamu haki zao katika misitu.



Mradi huo umeviwezesha vijiji zaidi ya 700 nchi nzima kupata elimu ya haki katika misitu ambapo vimegawanywa katika kanda mbalimbali.


Elinas Monga meneja mradi wa haki katika mazingira kutoka shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini TFCG amesema huu si wakati wa kufanya kazi kwa kujitolea tena kwa askari wa porini kutokana na fursa zilizopo katika misitu na changamoto ya uchumi iliyopo hivyo viongozi wa vijiji watumie fursa ya kuwepo kwa misitu kuwawezesha walinzi hao.

0 comments:

Post a Comment