Taifa
Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu)
alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja
kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions
of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Stars
iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na
imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa
Addis.
Kwa
mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya
kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan
Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.
Sudan
ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo
ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu)
dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0.
Wachezaji
wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris,
Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto
Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis
Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent
Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Kikosi
hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya
Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo
Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Addis Ababa
+251 919910240
0 comments:
Post a Comment