Rais Obama ametetea sera ya matumizi ya
ndege zisizokuwa na rubani katika kile
alichokiita vita halali.
Katika hotuba muhimu aliyoitoa kwenye chuo
kikuu cha ulinzi wa taifa cha Washington,
Obama alisema matumizi ya ndege hizo
yameifanya Marekani iwe salama zaidi.
Hata hivyo amesisitiza kwamba inapasa
kuhakikisha kuwa katika matumizi ya ndege
hizo hakuna raia anaeudhurika.
Rais Obama pia amesema utawala wake upo
tayari kukubali udhibiti zaidi wa mashambulio
yanayofanywa na ndege zisizokuwa na
rubani, nje ya maeneo ya vita kama
Afghanistan.
Amesema Marekani ipo vitani dhidi ya kundi
ambalo lingewaua Wamarekani wengi kwa
kadri ambavyo ingeliwezekana ,laiti hatua
zisingelichukuliwa kwanza kulizuia kundi hilo.
Juu ya juhudi za kuifunga jela ya
Guantanamo, Rais Obama alifahamisha
kuwa Marekani imeiondoa hatua ya
kuusimamisha kwa muda, mpango wa
kuwahamisha wafungwa na kuwapeleka
Yemen.
Katika hotuba yake kwenye chuo
kikuu cha ulinzi wa taifa mjini Washington,
Obama aliwaambia Wamarekani kwamba
jela ya Guantanamo imegeuka kuwa ishara
duniani kote, inayoonyesha jinsi Marekani
inavyokiuka sheria.
0 comments:
Post a Comment