MSANII Kala Jeremiah, kupitia wimbo wake Dear God
atachuana na Kigoma All Stars na wimbo wao Leka Dutigite kuwania tuzo ya wimbo
bora wa mwaka katika tuzo za Kilimanjaro, maarufu kama Kili Music Award baaaye
mwaka huu.
Akitaja majina ya washindania tuzo za mwaka huu, katika ukumbi wa Safari Pub uliopo ndani ya Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Ilala, Dar es Salaam Mwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Angelo Luhala aliwataja wengine wanaowania tuzo hiyo ni Mwasiti aliyemshirikisha Ally Nipishe katika wimbo Mapito Ommy Dimpoz aliyemshirikisha Vanessa Mdee katika wimbo Me n U na Ben Pol katika wimbo Pete.
Aidha, Luhala alisema Ben Pol atachuana na Diamond, Linex, Mzee Yussuf na Ommy Dimpoz kuwania tuzo ya Msanii Bora wa Kiume, wakati Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Lady Jaydee, Mwasiti na Recho watawania tuzo ya Msanii Bora wa Kiume.
Kwa upande wa tuzo ya Msanii Bora wa Kike Taarab, washindani ni Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Khadija Yussuf na Leila Rashid, waati tuzo ya Msanii Bora wa Kiume ya muziki huo wa mwambao itawaniwa na Ahmed Mgeni, Hashim Said na Mzee Yussuf.
Msanii Bora wa Kiume Bongo Fleva watachuana Ally Kiba, Ben Pol, Diamond, Linex na Ommy Dimpoz kwa msanii wa kike watapambana Linah, Mwasiti, Recho na Shaa na Msanii Bora wa Hip hop itakuwa ni kati ya Fid Q, Joh Makini, Kala Jeremiah, Profesa Jay na Stamina.
Msanii Bora wa Kiume Bendi watachuana Chaz baba, Dogo Rama, Greyson Semsekwa, Jose Mara na Khaleed Chokora na kwa msanii wa kike itakuwa kati ya Anneth Kushaba, Luiza Mbutu, Mary Lucos na Vumilia, wakati kwa Msanii Anayechipukia tuzo itawaniwa na Ally Nipishe, Angel, Bonge la Nyau, Mirror na Vanessa Mdee.
Video Bora ya wimbo wa mwaka, tuzo inawaniwa na Ommy Dimpoz (Baadae), Profesa Jay na Marco Chali (kamili Gado), Rich Mavoko (Marry Me), Bob Junior (Nichumu) na AY na Marco Chali (Party Zone).
Mtunzi Bora wa Mashairi ya Taarab; Ahmed Mgeni, Hemed Omary, Khadija Kopa, Mzee Yussuf, na Thabit Abdul, wakati Mtunzo Bora wa Mashairi ya Bongo Fleva Ally Kiba, Barnaba, Ben Pol, Linex na Ommy Dimpoz.
Mtunzi Bora wa Hip Hop; Fid Q, Joh Makini, Kala Jeremiah, Mwana FA na Stamina, wakati Mtunzi Bora wa Mashairi ya Bendi ni kati ya Chaz Baba, Semsekwa, Jonico Flower, Jose Mara na Khaleed Chokora.
Mtayarishaji Bora wa Mwaka; Bob Junior, C(, Ima The Boy, Man Water, Maneke, Marco Chali na Mensen Selecta, wakati kwa Mtayarishaji wa wimbo Bora wa Mwaka kwa bendi Ababuu Mwana Zanzibar atachuana na Allan Mapigo na Amoroso na Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka tuzo itawaniwa na D Classic, Imma The Boy, Mensen Selecta, Mr T Touch na Sheddy Clever.
Rapa Bora wa Bendi; Ferguson, Semsekwa, J$, Jonico na Sauti ya Radi.
Wimbo wenye vionjo vya Asili; Aambiwe wa Offside
Trick, Atatamani wa AT, Boma la Utete wa Young D, Chocheeni Kuni wa Mrisho Mpoto
na Dito na Mdundiko wa Momba na Juma Nature.
Wimbo Bora wa Bendi; Chanzi ni Sisi wa Mapacha Watatu, Jinamizi la Talaka wa Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde’, Risadi Kidole wa Mashujaa Band na Shamba la Twanga wa African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Wimbo Bora wa Reggae; Hii Si ya Waiga wa Yuzzo, Kilimanjaro wa Warriors From The East, Natafuta Paradise wa Mac Malick Simba, Salvation wa Delayla Princess na Tunda wa Hardmad.
Wimbo Bora wa Afrika Mashariki; Fresh All Day wa
Camp Mulla, Make You Dance wa Keko na Madtrax, Maswali ya Polisi wa DNA, Still
A Liar wa Wahu na Valu Valu wa Jose Chameleon.
Wimbo Bora wa Bongo Pop; Aifola wa LInex na Fundi Samuel, Baadae wa Dimpoz na Angel, Chuki Bure wa marehemu Sharo Milionea na Dully Sykes, Marry Me wa Mavoko na Me n U wa Dimpoz na Vannessa Mdee.
Wimbo Bora wa Kushirikiana; Chuki Bure,
Mapito, me n U, Sihitaji Marafiki nwa Fid Q na Yvonne na Single Boy wa Ally
Kiba na Lady Jaydee.
Wimbo Bora wa Hip hop; Alisema wa Stamina na Jux, Bum Kubam wa Nikki wa Pili na G Nako, Dear God, Nasema Nao wa Nay wa Mitego na Sihitaji Marafiki.
Wimbo Bora wa R&B; Amerudi wa Belle 9, Kuwa na
Subira wa Rama Dee na Mapacha, Maneno Maneno na Pete zote za Ben Pol.
Wimbo Bora wa Ragga na Dancehall; Je Ni Nani wa Ras Six, Muda Upite wa Susu Man, Predator wa Dabo, Push Dem wa Dr Jahson na Take It Down wa Chibwa na Tanah.
Wimbo Bora wa Zouk na Rhumba; Gubegube wa Barnaba,
Mapito, Nashukuru Umerudi wa Recho, Ni Wewe wa Amini na Sorry wa Barnaba.
Bendi Bora ya Mwaka; Africans Stars itachuana na Mapacha Watatu, Mashujaa, Mlimani Park na Msondo Ngoma, wakati Kundi Bora la Taarab, Dar Modern watachuana na Jahazi, Five Star, Kings na Mashauzi wakati kikundi bora cha muziki wa kizazi kipya tuzo inawaniwa na Jambo Squad, Makomando, Tip Top Connection, TMK Wanaume Family na Weusi.
Wasanii hawa wameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo baada ya mchakato wa akademi uliofanyika wiki iliyopita kuwapitisha na sasa watapigiwa kutafuta washindi.
0 comments:
Post a Comment