Main Menu

Wednesday, March 13, 2013

HATIMAYE PAPA MPYA APATIKANA NI KUTOKA ARGENTINA NA ACHAGUA JINA LA PAPA FRANCIS WA KWANZA

  
 

Hatimae Kanisa katoliki limempata kiongozi mpya atakaye chukuwa mahali pa Papa Benedict aliyejiuzuli.

Papa Mpya alichaguliwa katika duru ya tano ya upigaji kura uliofanywa na makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.

Maelfu ya watu walikusanyika eneo la St. Peters huko Vatican pamoja na dunia nzima walikua wakisubiri kujua jina la Papa mpya na ataamua kuchukuwa jina gani la Ki-Papa.
Hatimaye Jorge Mario Bergoglio kutoka dunia ya tatu amerika ya kusini nchini argentina amechagu Jina la Francis wa kwanza kuwa jina lake jipya.

 Shangaa usibishe huyu ni ndege wa kawaida tuingekua pale kwetu pale ingekua si bure kwa iman zetu






0 comments:

Post a Comment