Main Menu

Thursday, February 21, 2013

WAGHANA WAIANGAMIZA BARCA SAN SIRO, MATUKIO KATIKA PICHA

           Prince boateng akishangilia goli la kwanza kwa timu yake ya ac milan


       beki wa kati wa barca cales puyol pamoja na kujitoa kwa kila hali bado mambo yalikua magumu na mwisho wa siku alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na masherano
                                                      hapa sijaelewa ilikuaje
  mchezaji bora wa dunia lionel messi baada ya mchezo kumalizi wakiwa wamelala 2 bila
                   kocha wa club ya ac milan Massimiliano Allegriakiwa na furaha baada ya ushindi

                  Mario Balotelli akifurahina mpenzi wake ambaye ni mwana mitindo Fanny Robert Neguesha

wachezaji wa barca wakilalamikia goli la kwanza la ac milan kuwa kabla ya mpira kumfukia mfungaji ulishikwa




                         hii hali inakera

Baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Ac Milan usiku wa kuamkia leo kiungo wa Fc Barcelona Andres Iniesta amesema kuwa matokeo waliyoyapata yametokana na kikosi chao kutocheza vyema kikiwa ugenini.

Raia huyo wa Hispania amesema kufungwa magoli 2 kwa 0 na Milan kumewakosesha furaha kwakuwa hawakutegemea kupata matokeo hayo huku akisistiza kwamba timu yao ilicheza chini ya kiwango.

Kwaupande wake mlinzi wa Barcelona  Dani Alves ameonyesha  kuchukizwa  na matokeo hayo kwenye uwanja wa San Siro huku akijipa matumaini ya kufanya vyema katika mchezo wa maruadiano licha ya kukiri kuwa haitakuwa kazi rahisi.

Hatahivyo raia huyo wa Brazil amelalamikia goli la kwanza la Milan kwakusema kwamba kabla ya mpira kumfikia mfungaji mchezaji  Cristian Zapata aliugusa kwa mkono lakini mwamuzi hakuona tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment