mkuu wa wilaya ya iringa LETISIA WARIOBA akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji wa macho kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa iringa christine ishengoma.
mkuu wa wilaya ya iringa letisia warioba akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa kitengo cha macho hospital ya rufaa mkoa wa iringa
Kutokana na upungufu uliopo katika hospitali nyingi nchini, Wito umetolewa kwa watumishi wa idara ya afya mkoani Iringa kutumia vyema na kwa malengo yaliyokusudiwa vifaa vinayotolewa na wafadhili.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya iringa letisia warioba akimwakilisha mkuu wa mkoa katika uzinduzi wa jengo la upasuaji wa macho na kituo cha kupima na kutengeneza miwani uliofanika hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa.
Warioba amelishukuru shirika la Sightsavers na Brien Holden Vision Instute kwa ufadhili wa zaidi ya shilingi milioni 70 kwa ukarabati wa jengo la upasuaji na ununuzi wa vifaa tiba.

Mratibu wa macho mkoa wa Iringa Dr George Kabona, akitoa taarifa fupi ya huduma za mradi jumuishi wa macho mkoani humo, amesema mradi huo wenye sekta tatu za huduma za macho, elimu kwa wasioona na utengamao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa.
Aidha Kabona amesema kutokana na vifaa vilivyopatikana wanatarajia kuwafikia watu wengi zaidi tofauti na ilivyokua kipindi cha nyuma, huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo.
0 comments:
Post a Comment