Main Menu

Wednesday, January 16, 2013

KICHANGA CHATUPWA MAENEO YA CHUO CHA TUMAINI MKOANI IRINGA

Licha ya serikali pamoja na mashirika ya kutetea haki za bianadam kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, bado vitendo hivyo vimeendelea kuripotiwa kutokea sehemu mbalimbali nchini ambapo mkoani Iringa mtu mmoja ambaye hakufamika amemtupa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja.

Mtoto huyo amebainika kutupwa katika bonde la mto eneo la chuo kikuu cha Tumaini mkoani humo huku watu walioshuhudia tukio hilo wamelaani vikali na kutoa wito kwa serikali kuhakikisha inakomesha vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa kata ya Semtema B, Grace Masambula, akizungumza na Ebony Fm, mbali na kukiri kushudia tukio hilo, ameshindwa kubaini mtu aliyehusika na ukatili huo.


Hata hivyo baadhi ya mashuhuda waliofika katika eneo la tukio wamelaani kitendo hicho wakiwataka wanawake kuacha vitendo hivyo ambapo kwa upande mwingine wametupia lawama viongozi na jeshi la polisi kwa kufanya uzembe wa kufika katika eneo la tukio licha ya kupata taarifa mapema.

Mashuhuda hao wameeleza kuwa kichanga hicho kimetupwa majira ya alfajiri na kimeweza kubainika na mtu mmoja aliyekuwa akienda katika shamba lake lililopo karibu na bonde hilo
.

CHANZO EBONY FM

0 comments:

Post a Comment