Main Menu

Tuesday, January 15, 2013

KATIBU WA CCM MKANI IRINGA AMPIGA MWANDISHI WA HABARI MAHAKAMANI



KATIKA hali isiyo ya kawaida, katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Jackob Nkomola amefanya vurugu katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa , kwa kumvamia Mwandishi wa habari kwa kile alichokiita ni hasira ya kesi yake. 



Tukio hilo limetokea Leo majira ya saa tatu na nusu katika Mahakama ya Mwanzo iliyopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, baada ya katibu huyo kusomewa shtaka na hakimu wa Mahakama hiyo ya mwanzo Mh. Zakaria Mushi. 

Akisoma shtaka hlililomfikisha mahakamani hapo hakimu Mushi alisema mtuhumiwa Jackob Nkomola anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno, na hivyo kuvunja sheria kifungu namba 89 kifungu kidogo “A”. 



Aidha hakimu huyo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo, siku ya tarehe 3 mwezi wa kumi mwaka 2012 katika eneo la Mkombwe, ambapo alimtishia Alexandel Tweve  mkazi wa Mafinga. 


Mtuhumiwa alikana shtaka hilo na hakimu kutoa masharti ya dhamana ya ahadi ambayo inathamani ya shilingi  Laki mbili, na adhaminiwe na mtu mmoja atakayetambulishwa kwa barua kutoka katika ofisi ya serikali ya kijiji au Kata. 



Kupitia masharti hayo mshatakiwa alikuwa na mdhamini ambaye hakukidhi vigezo vya kuwa na barua  ya uthibitisho kutoka katika ofisi za serikali ya kijiji na hivyo kuzuiliwa kwa muda wa saa moja akiwa chini ya ulinzi, hadi kesi itakaposikilizwa tarehe 30 mwezi huu wa kwanza 2013. 



Hakimu alimtaka mstaki  wa kesi hiyo kufika na mashahidi wake aliowaorodhesha, na baada ya mwandishi wa gazeti hilo kutoka nje kwa ajili ya kupiga picha, mtuhumiwa alimfuata mwandishi na kumkuda akihoji ridhaa ya mwandishi huyo kupiga picha. 



“Kwa nini unanipiga picha?? Nani amekuruhusu unipige picha, kwanza wewe ni nani??, umepokea rushwa huko uje uniandike mimi, na nitaona kama habari hiyo itatoka,” Alihoji Katibu huyo. 



Akijibu maswali ya mtuhumiwa huyo mwandishi alisema “Mimi ni mwandishi wa habari, nimepata ruhusa kutoka kwa hakimu wa mahakama hii kufanya kazi yangu, na sijakupiga picha wewe, bali nilikuwa ninapiga picha ya kibao cha mahakama na jingo,”.



Hatua hiyo iliwashangaza watu waliohudhuria kesi hiyo katika viunga vya mahakama hiyo, wakihoji mamlaka ya mtuhumiwa kumfuata umbali wa hatua zaidi ya tano mwandishi, huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi kwa kuwa bado alikuwa naashikiriwa na Mahakama hiyo kwa kutokidhi vigezo vya dhamana yake.



Mwandishi alikimbilia kwa hakimu wa mahakama hiyo akitaka msaada juu ya tujkio hilo, na ndipo hakimu Mushi alimtaka mwandishi huyo kufika kituo cha polisi kutoa taarifa ya tukio hilo.



Akiwa njiani Mwandishi alimpigia simu Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi Cosmas Kaguo ambaye alimuomba mwandishi kuonana naye kabla ya kufika katika kituo cha Polisi cha Mafinga.



Hatua ya mwenyekiti wa CCM Kaguao, - aliitisha kikao cha dharua cha kamati ya siasa na kuomba radhi juu ya tukio lililotokea, na baada ya muda dakika 20 Katibu wa CCM (Mtuhumiwa) aliingia katika moja ya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, iliyopo katika ukumbi wa mikutano na kuomba radhi juu ya kile alichokifanya katika viunga vya mahakama.



Ombi la mwenyekiti wa CCM Wilaya, lilikubaliwa na mwandishi huyo kwa kusitisha hatua yake ya kufungua kesi katika kituo cha polisi Mafinga.



Akitoa utetezi wake, mtuhuimiwa huyo alisema “Ninaomba unisamehe sana Oliver, unajua kesi yangu hii niya kisiasa, na kukufanyia hivyo ni hasira baada ya mtu anayenituhumu kutumia njia mbalimbali za kuniangamiza, ninajua nimekukwaza wewe, lakini pia nimeidhalilisha taaluma yako, ninakuomba unisamehe,” Alisema Nkomola.



Hata hivyo wachagizaji wa masuala ya siasa Wilayani humo walisema katibu huyo amekuwa akitumia vibaya wadhfa alionao, na kujisahau kama kuna mikono ya sheria , na kuwa nguvu ya kufanya vurugu katika chombo hicho cha mahakama ambacho ni muhimili mkuu wa serikali, ni kutokana na jingo la Mahakama hiyo kuwa ni mali ya chama cha mapinduzi.



Kikao hicho cha usuruhishi dhidi ya tukio hilo, kilichukua zaidia ya saa nzima hadi kumalizika kwake, mwandishi huyo yupo wilayani humo kwa siku ya tatu sasa, akifuatilia masuala ya elimu kwa wanafunzi wanaoanza elimu ya kidato cha kwanza, pamoja na changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu na Kilimo Wilayani humo.

0 comments:

Post a Comment