Main Menu

Friday, January 18, 2013

CHEKI PICHA ZA NDEGE AINA YA BOEING 787 DREAMLINER ZILIZOSIMAMISHWA



















Ndege zote aina ya Boeing 787 Dreamliner zimesimamishwa hadi pale matatizo yanayoweza kusababisha moto yatakapokuwa yamepatiwa ufumbuzi. 

Nchi mbali mbali zikiwemo Chile, India, Qatar, Ethiopia na Umoja wa Ulaya zimefuata hatua ya Marekani, baada ya ndege mbili za aina hiyo zinazomilikiwa na shirika la ndege la Japan kutua katika hali ya dharura Jumatano. 

Wataalam wanakadiria kuwa itachukua muda wa wiki kadhaa kurekebisha makosa katika ndege hiyo ya kimarekani iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu. 

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Boeing Jim McNerney amesema kuwa kampuni hiyo inasikitishwa na usumbufu uliotokana na hitilafu hizo, na kuahidi kufanya kila juhudi kulimaliza tatizo hilo haraka.

0 comments:

Post a Comment