TAARIFA YA KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI YA
ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JANUARI 05, 2014
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia
abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa
kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa
kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014
saa 3 usiku imeahirishwa hadi kesho
Jumapili Januari 05 Machi 16, 2013, saa
3 usiku.
Taarifa imefafanua kuwa kutokana na mvua kunyesha mkoani
Dodoma na mikoa jirani eneo kati ya
stesheni za reli ya kati za Gulwe na Godegode zimejaa maji na kufunika njia ya
reli mkesha wa mwaka mpya wa 2014!.
Tokea juzi Januari 02, 2014 Wahandisi na mafundi wa kampuni za
TRL na Rahco kwenye sehemu husika wakifanya tathmini na kusimamia ukarabati wa maeneo mawili reli yaliyoharibika.
Kwa mujibu Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo
Amani Kisamfu anayeongozwa kikosi kazi cha kukarabati amesema kazi ya ukarabati
inafanywa usiku na mchana kuona huduma zinaanza mapema iwezekanavyo ikiwemo huduma
ya usafiri wa treni za abiria uliopangwa kuanza tena hapo
kesho Jumapili Januari 05, 2014.
Kutokana na dharura hii treni za kutoka Mpanda, Kigoma na
Mwanza kuja Dar zimebadilishiwa muda na siku ya kuondoka hivyo basi, badala ya kuondoka jana Ijumaa Januari 03,
2014 sasa zitaondoka kesho Jumapili Januari 05, 2014 saa 2 asubuhi.
Aidha taarifa hii
iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa
TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..
Imetolewa
na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal
Mafikiri.
TRL Makao
Makuu,
Dar es
Salaam.
Januari
04, 2014
0 comments:
Post a Comment