Main Menu

Friday, August 16, 2013

MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA KAMATI YA UENDESHAJI YA MATOKEO MAKUBWA SASA (BIG RESULT NOW) YA SEKTA YA UCHUKUZI LEO


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) kufungua mkutano wa kwanza wa kamati ya Uendeshaji  ya Matokeo makubwa sasa katika sekta ya Uchukuzi, leo katika ukumbi Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Wajumbe wa kamati ya Uendeshaji ya Matokeo Makubwa sasa (Big Result Now) ya sekta ya Uchukuzi wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(hayupo pichani), wakati Waziri huyo alipofungua mkutano wa kwanza wa kamati hiyo leo  katika ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya Matokeo makubwa sasa(Big Result Now) kwa sekta ya Uchukuzi, wakati alipokutana na kamati hiyo leo mchana katika ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Gerson Lwenge. Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kusimamia utekelezaji wa Matokeo makubwa sasa iliyopo chini ya Ofisi y Rais, Bw. Omar Issa.
 Mratibu wa Miradi iliyo kwenye mpango wa Matokeo makubwa sasa katika sekta ya Uchukuzi, Bw. Aunyisa Meena akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa kamati ya Uendeshaji katika sekta ya Uchukuzi, leo mchana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli(RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito akifafanua hatua iliyofikiwa kwenye miradi ambayo iko kwenye Mpango wa matokeo makubwa sasa katika sekta ya uchukuzi, wakati wa mkutano wa kwanza wa kamati ya uendeshaji katika sekta ya Uchukuzi,uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.  


PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINII UCHUKUZI


0 comments:

Post a Comment