Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba nchini Misri
leo ameapishwa kuwa rais mpya wa kipindi cha mpito
na kuchukuwa madaraka masaa kadhaa baada ya
jeshi la nchi hiyo kumpindua Rais Mohamed Mursi.
Jaji Adly Mansour amekula kiapo hicho katika makao
makuu ya Mahakama ya Katiba yaliyoko pembezoni
mwa Mto Nile mjini Cairo katika hafla iliyotangazwa
hewani moja kwa moja na televisheni ya taifa.
Kwa
mujibu wa agizo la kijeshi Mansour atakuwa kiongozi
wa serikali ya mpito nchini Misri hadi hapo rais mpya
atakapochaguliwa.
Tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi
mpya bado haikutangazwa.
Mursi ambaye alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa
kidemokorasia nchini humo mwaka mmoja uliopita
amekuwa kwenye kifungo cha nyumbani katika
mahala ambako hakukutajwa tokea majenerali
wamuondowe madarakani hapo jana katika kile
wafuasi wake walichokiliaani na kukiita kuwa ni
mapinduzi ya kijeshi.
Takriban washauri na wasaidizi
wake kadhaa pia wako katika kifungo cha nyumbani.
Waendesha mashtaka wameamuru kukamatwa kwa
viongozi waandamizi chama cha Udugu wa Kiislamu.
Dw swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment