Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi watakaochezesha mechi
ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na Barrack Young
Controllers II ya Liberia itakayochezwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Mwamuzi
wa kati ni Adelaide Ali, mwamuzi msaidizi namba moja ni Amaldine
Soulaimane wakati Ibrahim Mohame atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.
Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ansudane Soulaimane.
Kamishna
wa mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni atakuwa Abdelhamid Radwan
kutoka Misri. Maofisa hao wa mechi hiyo watafikia kwenye hoteli ya
Holiday Inn.
Wakati
huo huo, Barrack Young Controllers II imewasili nchini leo (Aprili 2
mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi,
Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra,
Ghana.
Timu
hiyo iliyofia hoteli ya Sapphire Court itafanya mazoezi leo jioni
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake
kwa ajili ya mechi hiyo huku wapinzani wao Azam wakiendelea kujinoa
kwenye uwanja wao wa Azam Complex.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment