Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani
Baba Mtakatifu Benedict wa 16 amejiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter.
Tarehe 3 dec mwaka huu 2012 Baba Mtakatifu alifungua ukurasa huo kwa lugha
ya Kiingereza ambao tayari umekwisha wavutia watu 92,000.
Idadi hii inatarajiwa kuongezeka
mara kiongozi huyo mzaliwa wa Ujerumani atakapoandika kitu kwenye ukurasa huo.
Bado hajasema chochote hadi sasa
tangu kuufungua.
Uongozi wa Vatican umesema kuwa
ataanza kuutumia rasmi tarehe 12 mwezi huu.
Hadi sasa kurasa nane za mtandao wa
Twitter zimeshafunguliwa chini ya jina ya baba mtakatifu Benedict wa 16 zikiwa
kwenye lugha mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment