Main Menu

Thursday, July 9, 2015

RAHEEM STERLING AITOSA TENA LIVERPOOL MAZOEZINI

Raheem Sterling and Brendan Rodgers

Winga wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling ameshindwa tena kufanya mazoezi na timu yake ya Liverpool  hii leo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa mchezaji huyo bado anasema kuwa anaumwa na hakufanya mazoezi.

Hapo jana Sterling alishindwa kufanya mazoezi na wenzake kwa kusema kuwa anaumwa na taarifa zikazidi kusema kuwa mchezaji huyo hatojiunga na timu kwa maandalizi ya msimu ujao wa  Ligi ambayo yataanzia nchini Thailand.

Daktari toka Liverpool alikwenda kuangalia Afya yake na kupendekeza aina ya matibabu anayopaswa kufanyiwa Raheem Sterling.

Kwa muda mrefu sasa mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester City.

0 comments:

Post a Comment