Main Menu

Thursday, June 25, 2015

VILLA YAWASILI KUWAVAA YANGA, MASHABIKI MAN U, YANGA WAJINOA PIA


 
Mabingwa wa Uganda timu ya Sports Club Villa imewasili nchini leo mchana tayari kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa hisani dhidi ya yanga siku ya jumamosi.

Mratibu wa mchezo huo ambao mapato yake yatasaidia ujenzi wa kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi Mosi Magere amesema waziri mkuu mizengo panda ndiye atakayekua mgeni rasmi katika mchezo huo.

Mchezo huo utatanguliwa na mchezo wa mashabiki wa Manchester United dhidi ya mashabiki wa Yanga.

Timu ya mashabiki wa manchestar united itaongozwa na Chicharito, Shaffih Dauda, Sebo,Yahaya Mohamedy, Jeflea, Mbwiga, Kawambwa, na Tupatupa.

Wakati yanga mashabiki wataongozwa na Maulid Kitenge, Aron Nyanda, Ally mayai, Omary Katanga, Masudi Kipanya na Ray Kigosi.

Band ya Yamoto itakuwepo kwa ajili ya kutoa burudani uwanjani hapo.

Makocha wa timu zote mbili kesho wanatarajiwa kukutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuzungumzia mchezo huo wa jumamosi.

0 comments:

Post a Comment