Main Menu

Thursday, June 11, 2015

KWA MTINDO HUU KUKUA KWA SOKA LA TANZANIA TUSUBIRI MIAKA MIA NANE



Bodi ya ligi Tanzania kwa kushirikia na wadhamin wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom usiku huu imetoa tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi hiyo.

Kulikua na vipengele vitano vilivyokua vinashindaniwa ambavyo ni mchezaji bora wa msimu, golikipa bora, mwamuzi bora, timu yenye nidhamu na kocha bora.
 
Nafasi ya bingwa na zile nafasi zingine za juu zenyewe zilishajulikana kama ilivyokua na mfungaji bora.

Pamoja na kulalamikiwa tangu pale walipotajwa majina ya washiriki, leo bado bodi ya ligi imeendelea kuwashangaza watu kwa kumteua mbwana makata kuwa kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita.

Makata alikua anachuana na kocha wa yanga hans van pluijm pamoja na aliyekua kocha wa Simba Kopunovic.
 Wazazi wa Simon Msuva wakiwa wameshika tuzo ya mtoto wao mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mh. Juma Nkamia
Wazazi wa Simon wakipokea tuzo za mwanae ambaye yupo na timu ya taifa Ethiopia.

Tuzo ya mchezaji bora imekwenda kwa Simon Msuva baada ya kuwaangusha Mrisho Ngassa, na Mohamed Husein Shabalala.

Kipa bora amepewa shaban Hassan Kado, wakati timu yenye nidhamu imepewa mtibwa sugar.
Shabani Kado akipokea tuzo yake
Mwamuzi wa msimu ni Israel Mujuni Nkongo.

Mgeni rasmi katika tuzo hizo alikua naibu Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na michezo mh Juma Nkamia.

0 comments:

Post a Comment