Main Menu

Thursday, June 18, 2015

DIDIER KAVUMBAVU ATOA SABABU ZA KUTOFANYA VIZURI MZUNGUKO WA PILI



 Kocha wa viungo wa Azam Fc Mario Marineka (kushoto) Jaffar Idd Maganga na didier Kavumbagu (kulia) baada ya mazoezi.



Mshambuliaji  wa timu ya Azam Fc mrundi Didier Kavumbagu ametoa sababu za kushindwa kufanya vizuri katika msimu wa pili wa ligi kuu uliomalizika mwezi uliopita.

Akizungumza na mtandao huu kavumbagu amesema mabadiliko ya mwalimu ndio sababu kubwa na yeye kushindwa kufanya vyema mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom.

Ikumbukwe wakati ligi inaelekea mzunguko wa pili Kavumbagu alikua na magoli kumi lakini alijikuta akishindwa kupasia nyavu tena na kumpa nafasi Simon Msuva na Amisi Tambwe kumpita.

Didier amesema sababu nyingine ni ya kifamilia ambayo ilimfanya wakati mwingine akili yake kutokua vyema na kushindwa kupaform.

Katikati mwa msimu uliopita Azam Fc walimtimua kocha wake Mcameroon Joseph Omog baada ya timu hiyo kushindwa kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa ya klabu bingwa afrika baada ya kutolewa na El Merrekh ya Sudan.

Kavumagu ndie mchezaji pekee wa kigeni aliyejiunga na kikosi cha Azam kilichoanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kagame.

0 comments:

Post a Comment