Main Menu

Wednesday, May 20, 2015

SPORTS XTRA NDONDO CUP YAANZA KWA KUKAMIANA



 
Sports Xtra Ndondo Cup , mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za mitaani za jiji la dar  es salaam yameanza leo kwa hatua ya awali.

Michezo ya ufunguzi leo imefanyika katika viwanja vinne vya Kinesi, Mizinga, Airwing na Benjamin Mkapa.
 
Katika michezo hiyo ya ufunguzi Vijibweni city wamekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa  Wakung’aza Fc katika dimba la mizinga kigamboni.

Wazee wa vigoma Santiago Chile wametoa kipigo cha bao 3-0 kwa Kisarawe Rangers pale shule ya Benjamin Mkapa.

Faru Jeuri wakaishindilia Kisarawe United bao 4-0 pale jeshini airwing Ukonga, na Sindano Fc ikachapwa 1-0 na No Star uwanja wa Kinesi Sinza.

Michezo hiyo itaendelea tena kesho kwa Mbagala city vs Mjivuni fc, Tuamoyo fc vs Toangoma fc, Sharif united vs Kivule united na Faru Dume vs Kimara united.

0 comments:

Post a Comment