Main Menu

Friday, May 29, 2015

RASMI: AZAM FC YATAJA SAFU YAKE YA UONGOZI



Klabu ya Azam FC imefanya mabadliko makubwa ya watendaji na kidogo kwenye mfumo wake wa uongozi, ili kuleta tija na mafanikio kwa haraka katika klabu hiyo.

taarifa ya klabu hiyo kupitia ukurasa wake ya facebook imesema Utekelezaji wa mabadiliko hayo unaanza mwezi huu.

BODI YA WAKURUGENZI;
Hiki ni kikao cha juu kabisa cha maamuzi ya klabu, wajumbe wake wanabaki kuwa wanafamilia wa familia ya Bakhresa.


 Viongozi na baadhi ya watendaji hualikwa kwenye vikao ili kutoa ripoti za utendaji na sera.

UONGOZI;
Mwenyekiti wa klabu anabaki kuwa mzee Said Muhammed, huku aliyekuwa katibu mkuu wa muda mrefu tangia klabu ianzishe Nassor Idrissa “Father” akipanda ngazi moja na kuwa Makamo Mwenyekiti. 


Nafasi ya katibu mkuu imefutwa. Nafasi ya Ukurugenzi wa Sheria na haki za wachezaji inaendelea kushikiliwa na mwanasheria Shani Christoms.

WATENDAJI:
Mtanzania Saad Kawemba anaendelea kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu huku klabu ikimuajiri muingereza mwenye asili ya Uganda Eli Eribankya kuwa Meneja utawala na fedha. 


Eribankya atasaidiwa na mwanandinga wa zamani wa Azam FC mtanzania Luckson Kakolaki. 

BENCHI LA UFUNDI
Stewart John Hall kutoka uingereza anarejea kwa mara ya tatu kuongoza benchi la ufundi la Azam FC. 


Hall atasaidiwa na Mganda George Best Nsimbe, huku Mark Philips kutoka uingereza akiajiriwa kuwa kocha wa magolikipa.

Aliyekuwa kocha wa magolikipa kwa muda mrefu Iddi Abubakar ataendelea kuwepo kama msaidizi wa Mark Philips.

Mtaalamu wa tiba ya viungo na lishe “Team Physiotherapist and Nutritionist” atakuwa George Adrian Dobre kutoka Romania na Yusuf Nzawila ataendelea kuwa Kit Manager. 

Timu bado inatafuta Daktari na mtaalamu wa tiba ya viungo “Physiotherapist” 

BENCHI LA UFUNDI LA ACADEMY
Mario Marian Anton Marinica kutoka Romania ataongoza benchi la ufundi la timu ya vijana akisaidiwa na Mtanzania Dennis Kitambi na Idd Nassor Cheche. 


Twalib Mhidin ataendelea kwa msaidizi wa Team Dr kwa vijana na mtunza vifaa msaidizi vya vijana atakuwa Saleh Sale

0 comments:

Post a Comment