Main Menu

Friday, May 15, 2015

KATIBU MKUU SIMBA AACHIA NGAZI



Siku chache baada ya wachezaji wawili wa timu ya simba kutangaza kuachana na timu hiyo, Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally naye ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya madaktari wa Muhimbili kumshauri kupumzika kwa muda usiojulikana kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo.

Stephene aliingia madarakani mwaka jana kuchukua nafasi ya Ezekiel kamwaga mara baada ya uongozi mpya kuingia madarakani kuiongoza timu hiyo chini ya Rais Evans Aveva.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Stephene amesema kikubwa kilichomfanya ajiuzulu ni kutokana na matatizo ya kiafya.

0 comments:

Post a Comment