Main Menu

Monday, January 21, 2013

UKUTA WAANGUKIA MAGARI, WAJERUHI WATATU KITUO CHA MABASI UBUNGO



Hali ilikuwa ni mbaya katika zahama hiyo ya alfajiri ya leo.
Hii ndiyo hali halisi ya tukio lilivyokuwa.
Kenyela akiongea jambo Juu ya ajali hiyo.
Watu wakiangalia magari yao
Gari aina ya Toyota likiwa limebonyezwa na zege.
Gari aina ya Toyota likiwa limebonyezwa na zege.
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.
Magari mbalimbali yakiwa chini ya kifusi.
Baadhi ya magari yaliyoangukiwa na ukuta.
Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo
Mkatisha ushuru wa maegesho hayo akiendelea kukusanya ushuru.
chanzo vijimambo

0 comments:

Post a Comment