Main Menu

Tuesday, August 27, 2013

MAN UNITED, CHELSEA 0-0, ROONEY ANG'ARA


KOCHA wa Manchester United, David Moyes amepeleka ujumbe kwa Chelsea kwamba Wayne Rooney hatahamia Stamford Bridge majira haya ya joto kufuatia mchezo wa jana wa miamba hao uliomalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Old Trafford. 
 
Rooney alianza katika kikosi cha kwanza baada ya tetesi za muda mrefu majira haya ya joto kwamba atajiunga na Jose Mourinho Magharibi mwa London, lakini alipiga soka ya uhakika akiwa na uzi mwekundu. 
Chelsea's Ramires is challenged by Manchester United's Wayne Rooney
Rooney akimdhibiti Ramires  
Chelsea ilianza bila washambuliaji wake Fernando Torres na Romelu Lukaku walioanzia benchi, lakini gumzo zaidi ni kila upande kulalamikia kunyimwa penalti katika mechi hiyo.

Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu, Welebeck, Rooney na Van Persie.
 
Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa 'akapeta'. 
 
Dakika ya 71 Ashely Cole alianguka kwenye eneo la hatari wakati akikabiliana na Jones na akalilia penalti na hata Mournho akaonekana kulalamika akiwa kwenye benchi.  
 
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo zilishambuliana kwa zamu na baada ya mechi wachezaji walipongezana kwa mchezo mzuri.
 
Jose Mourinho alisema baada ya mechi mchezo ulikuwa wa haki na hadhani kama kuna iliyomzidi mwenzake uwezo, wakati Moyes alilalamikia penalti ya Lampard kuunawa mpira na kuwapongeza vijana wake kwa soka nzuri.
 
Kikosi cha Man United kilikuwa: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia/Young dk67, Cleverley, Carrick, Welbeck/Giggs dk78, Rooney na Van Persie.
 
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne/Torres dk60, Oscar, Hazard/Azpilicueta dk93 na Schurrle.
Back in the fold: Rooney started for United but was unable to break the deadlock at Old Trafford
Amerudi kikosi cha kwanza: Rooney alianza katika kikosi cha kwanza na alicheza vizuri akipiga mashuti mazuri mawili yaliyokaribia kuzaa mabao Old Trafford
Rough and tumble: Cole scythes RVP down during an entertaining but goalless first-half
Rafu: Cole akimchezea rafu RVP 
Rough and tumble: Cole scythes RVP down during an entertaining but goalless first-half
Cole akimdhibiti RVP 
Handball? The Old Trafford faithful were on their feet asking for a penalty after the ball hit Lampard's hands
Mpira wa mikono? Lampard akiwa ameshika mpira kwa mikono ndani ya eneo la hatari na refa hakutoa penalti, ingawa anashuhudia tukio hapo
Handball? The Old Trafford faithful were on their feet asking for a penalty after the ball hit Lampard's hands
Kipa? Lampard alibeba majukumu ya kipa wake dakika ya 65
Dive? Cole incensed the home fans after taking a tumble under very little contact from Jones
Alijirusha? Cole alianguka kwenye eneo la hatari na kulilia penalti, wakati akikabiliana na Jones
Dive? Cole incensed the home fans after taking a tumble under very little contact from Jones
Analilia penalti: Kocha Jose Mourinho akilalamika baada ya Cole kuanguka na refa hakutoa penalti
New era, new boss: Moyes found his place in the United dugout and was given a warm welcome by the fans
Zama mpya, kocha mpya: Moyes akiiongoza United leo baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu
New era, new boss: Moyes found his place in the United dugout and was given a warm welcome by the fans
Mapokezi mazuri; Moyes akisaini karatasi za mashabiki
Staying game: Rooney is wanted by Chelsea but was promoted to the starting XI to face his suitors
Rooney anatakiwa na Chelsea, lakini leo alipandishwa kikosi cha kwanza
Staying game: Rooney is wanted by Chelsea but was promoted to the starting XI to face his suitors
Cole akikabiliana na Rooney
Warm welcome: Mourihno and Moyes embraced before kick-off at Old Trafford
Mourihno na Moyes wakisalimiana kabla ya mechi Old Trafford

0 comments:

Post a Comment