Main Menu

Wednesday, August 13, 2014

KOCHA PATRICK PHILI ATUA NCHINI KUCHUKUA NAFASI YA LOGA MSIMBAZI

 Kocha mpya wa Simba Patrick Phiri amewasili leo nchini tayari kwa kuanza kibarua kwa mara ya tatu tofauti katika timu hiyo yenye maskani yake Jijini Dar es Salaam.


Kocha huyo amewasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere majira ya saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Fast Jet na kulakiwa na Viongozi wa timu hiyo.

Phiri anatarajia kusaini mkataba ambao bado haujawekwa wazi utakuwa wa muda gani kabla ya kuanza kibarua rasmi cha kuinoa timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Zambia anachukua nafasi ya Mcroatia Zdravko Logarusic alietimuliwa mwishoni mwa juma, baada ya timu hiyo kuchapwa mabao matatu kwa sifuri na Zesco ya Zambia siku ya Simba Day.


0 comments:

Post a Comment