Main Menu

Tuesday, May 26, 2015

HARUNA CHANONGO AIKANA YANGA, BADO YUPO NJIAPANDA



 
Haruna Chanongo akiwa ndani ya uzi wa timu ya taifa (taifa stars)
Winga Haruna Chanongo wa Stand United ameikana Yanga baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba mchezaji huyo amesaini kuichezea timu hiyo.

Chanongo aliyekua anaichezea Stand United kwa mkopo kutoka Simba alihusishwa kusajiliwa na Yanga pamoja na mchezaji Dues Kaseke siku ya jumapili.

Akizungumza na mtandao huu chanongo amesema hajasaini kuichezea yanga japo mazungumzo yalianza kufanyika baina ya viongozi wa yanga na wakala wake lakini muafaka bado haujafikiwa.

Kuhusu kwenda kufanya majaribio kunako timu ya Tp mazembe  Chanongo amesema majeruhi ndio sababu ya yeye kushindwa kwenda  DR Congo kufanya majaribo.

Hata hivyo kumekuwepo na taarifa nyingine kwamba Azam Fc wamejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kumtaka mchezaji huyo aliyemaliza mkataba na timu yake ya Simba.

0 comments:

Post a Comment