
Murry alianza mpambano huo akiwa vizuri na alibaki hivyo hadi mwisho, japo alionesha kupatwa na mshangao kutokana na ushindani mkali aliokutana nao kutoka kwa mpinzani wake huyo.
Sasa Murray anataraji kuvaana na Nick Kyrgios kutoka Australia.
"nilifurahi sana namna nilivyobadili mchezo na kuweza kufanya marekebisho pale uwanjani, ambapo upepo mzuri ukahamia kwangu" alisema Murray.
Naye Muingereza mwingine Heather Watson, amegaragazwa na Mmarekani Sloane Stephens kwa set 6-2 6-4, huku Rafael Nadal na Novak Djokovic wakifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua hiyo ya tatu.
0 comments:
Post a Comment