Main Menu

Friday, April 24, 2015

YANGA UBINGWA ULEEEE, YAISHINDILIA RUVU SHOOTING 5 BILA



Kwa zaidi ya asilimia 90 unaweza ukasema yanga ndio mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa mwaka 2014/2015.

Hii inatokana na matokeo waliyoyapata hii leo dhidi ya timu ya Ruvu Shooting kutoka mkoani pwani katika muendelezo wa ligi kuu, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo yanga imeibuka na ushindi wa mabao 5 kwa bila na hivyo kuhitaji alama 3 tu kuwavua ubingwa watetezi wa taji Azam Fc.

Yanga sasa imefikisha alama 52 zikiwa ni 10 mbele ya Azam Fc japo Yanga ina mchezo mmoja mkononi.

Magoli ya Yanga hii leo yamefungwa na Simon Msuva na Kpah Sherman waliofunga magoli mawili kila mmoja pamoja na goli la Amisi Tambwe.

Kwa magoli hayo Msuva amefikisha magoli 16 na kujikita kileleni mwa wafungaji huku Tambwe akifikisha magoli 11 katika nafasi ya pili.

Ligi hiyo itaendelea kesho ambapo Azam Fc itawaalika Stand United, Simba Sc itakua mwenyeji wa Ndanda fc, na Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar.

0 comments:

Post a Comment