Main Menu

Friday, April 17, 2015

MWENYEKITI WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA AWAPA MAKAVU TFF



Mwenyekiti wa baraza la michezo la Taifa, Dioniz Malinzi amelitaka shirikisho la soka nchini kuwawajibisha waamuzi wanaoharibu mpira wa miguu nchini.

Malinzi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya waamuzi vijana 35 kutoka mikoa mbalimbali nchini yaliyokua yanafanyika katika uwanja wa Karume Dar  es salaam.

Amesema haiwezekani viongozi wa TFF wanakuwepo uwanja wa taifa na waamuzi wanaruhusu magoli yasiyo halali nab ado katika mchezo ujao unawaona tena wapo katikati ya uwanja kisa unasubiri ripoti ya msimamizi.

“Tuna matatizo mengi katika michezo lakini tatizo kubwa ni waamuzi ambao wanatuharibia mpira wetu kwa sababu ya tamaa  na ubinafsi badala ya kuwafikiria watanzania wanafikiria matumbo yao”amesema malinzi.

Malinzi amefika mbali zaidi hadi kuhoji au viongozi hao nao wanapewa mgao wa rushwa wanaopewa waamuzi kwa sababu haiwezekani ukashuhudia upuuzi wa waamuzi na  bado ukakaa kimya  bila kuchukua hatua yoyote.

“Ni kazi bure timu kutumia mamilion ya fedha kujiandaa alafu mwisho wa siku anakuja mtu mmoja kusimama katikati ya uwanja na kuharibu ladha ya mchezo kwa kutoa maamuzi yasiopendeza”amesema.
Mwenyekiti huyo amesema itakua ni kazi bure kuwaandaa vijana wadogo kuwa waamuzi alafu wanawaona wakubwa wao wanaharibu mpira na wahachukuliwi hatua yoyote.

Amesema mpira ni mali ya TFF na sio bodi ya ligi wala kamati ya waamuzi, hivyo chochote kitakacho haribika wakuulizwa ni TFF, hivyo ameitaka TFF iwe strong kusimamia mpira na kuondoa upuuzi wote unaoendelea.

“Haiwezekani televishen zimeonesha, viongozi wa TFF walikua uwanjani wameona madudu ya waamuzi alafu kwenye ripoti hakuna maelezo yanayoeleka na bado mnaakaa kimya haiwezekani”amesema.

Mwisho Dioniz Malinzi amelitaka shirikisho hilo kuboresha maslahi ya waamuzi labda inaweza kupunguza ushawishi wa kupokea rushwa kwani haiwezekani mchezo uingize sh. million 70 mwamuzi anapewa laki mbili…..tena anasafirishwa kwa basi kutoka Musoma kuja dar.

Kamaliza kwa kuwahusia vijana hao kuwa mbali na rushwa kwa sababu rushwa ni adui wa haki.

0 comments:

Post a Comment