Main Menu

Thursday, April 9, 2015

KUMUONA KLUVERT, PUYOL, GARCIA, DECO NA WENGINE BUKU 7,000/=



Wakati wachezaji wakongwe wa klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania wakiwa wameshawasili nchini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven, viingilio vya mpambano huo vimetajwa.

Viingilio hivyo vimegawanywa katika mafungu matano ambapo VIP A ni shilingi 300,000, VIP B sh. 100,000, VIP C sh. 30,000 wakati jukwaa la Orange itakua sh. 20, Jukwaa la Blue sh. 10,000 na jukwaa la Kijani ni sh. 7,000.

Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya ijumaa asubuhi katika vituo vya uwanja wa karume, Break Point maeneo ya posta mjini, Dar live Mbagala, Buguruni Sheli, Ubungo oil com, Makumbusho stand, Feri kigamboni na Feri upande wa kivukoni, Uwanja wa taifa, Mlimani city, na NPS (National Parking System wa mjini nao watauza tiketi pia.

Pambano hilo litafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 11 April katika uwanja wa taifa jijini Dar  es salaam kuanzia saa kumi kamili jioni.

Timu hiyo ya wakongwe wa Barcelona imeanza kuwasili nchini wiki iliyopita kwa kutangulia kocha wake Johan Cryuff ambapo baada ya kukamilika walitembelea hifadhi ya Serengeti na kisha visiwani Zanzibar kwenye mualiko wa rais wa huko Dr. Mohamed Sheni.

0 comments:

Post a Comment