Main Menu

Tuesday, April 14, 2015

ERIC CANTONA AIPA UBINGWA MAN U MSIMU UJAO.



Shujaa wa zamani wa timu ya Manchester United Eric Cantona amefurahishwa na ushindi walioupata Man U wikiendi iliyopita katika ile Manchester Derby na sasa anaamini timu hiyo msimu ujao wa 2015/2016 itatwaa ubingwa wa EPL.

Legendary huyo aliyeichezea Man U miaka ya tisini anaamin timu yake itashinda taji la ligi msimu ujao.

Louis van Gaal na vijana wake wanashika nafasi ya tatu wakiwa  pointi nane nyuma ya viongozi Chelsea, kufuatia ushindi wa michezo sita mfululizo waliupata na kuwaweka umbali wa point nne juu wa timu inayoshika nafasi ya nne na alama nane kwa timu inayoshika nafasi ya tano.

Kwa hali hiyo united ina nafasi ya kumaliza katika nafasi nne za juu na kushiriki ligi ya mabingwa baada ya kuikosa msimu uliopita.

Cantona ametoa kauli hiyo alipokua akizungumza katika tuzo za  Laureus World Sports jijini  Shanghai mapema leo.


Mfaransa huyo ambaye alishinda makombe manne ya ligi kuu na mawili ya kombe la FA katika kipindi cha mika mitano Old Trafford, alifurahishwa sana na ushindi wa Red Devils dhidi ya mpinzani wake wa jadi Manchester City siku ya Jumapili.

0 comments:

Post a Comment