Main Menu

Tuesday, March 17, 2015

TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER KUIFUATA ALHAMISI



Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kuodoka siku ya alhamisi kuelekea jijini Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa soka la ufukweni utakaofanyika siku ya jumapili.

Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Misri utakaofanyika siku ya jumapili jijini Cairo ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli kufuatia kupoteza mchezo wake awali uliofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Msafara wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na shirika la ndege la Ethiopia, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, kocha mkuu John Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja Deogratius Baltazar na daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.

Wachezaji ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus Kessy, Samwel Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima, Mwalimu Akida Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby Abdallah.

0 comments:

Post a Comment