Main Menu

Friday, March 20, 2015

BEACH SOCCER YAWASILI SALAMA MISRI



Timu ya Taifa ya soka la Ufukweni (Beach Soccer) imewasili salama jijini Cairo nchini Misri tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli.

Msafara wa timu ya soka la Ufukweni ulipokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania waliopo nchini Misri,  pamoja na viongozi wa chama cha soka nchini Misri (EFA).

Leo jioni kikosi kinatarajia kufanya mazoezi mepesi, kabla ya kesho kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja utakaofanyika mchezo siku ya jumapili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaitakia kila la kheri timu ya soka la ufukweni katika mchezo wake wa marudiano siku ya jumapili dhidi ya Misri.


FAINALI SDL JUMATATU

Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kufanyika siku ya jumapili katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam siku ya jumatatu Machi 23 mwaka huu kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mchezo huo wa fainali utazikutanisha timu za Mbao FC ya Mwanza dhidi ya Kiluvya United FC ya Pwani, ambapo mshindi wa mchezo ndio atakua Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Pili.


Jumla ya timu nne tayari zimeshapanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutoka Ligi Daraja la Pili (SDL) ambazo ni Kiluvya United ya Pwani, Mji Njombe ya Njombe, Mbao ya Mwanza na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma.

0 comments:

Post a Comment