Main Menu

Wednesday, March 11, 2015

ALIYEKUA KOCHA WA NDANDA FC ATEULIWA KUWA KOCHA MSAIDIZI AZAM FC

Aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ndanda Fc mwanzoni mwa msimu huu na baadae kutimuliwa kutokana na mwenendo usioridhisha Denis Kitambi amepewa deal la kuwa kocha msaidizi wa timu ya Azam fc.

Kitambi baada ya kutimuliwa Ndanda Fc alikuangukia kwenye uchambuzi wa soka, ambapo awali alianza na kituo cha Clouds fm na Tv kabla ya kuhamia Azam Tv ambao kimsingi ipo ya mwamvuli mmoja na timu ya Azam.

Kitambi analamba deal hiyo baada ta azam kumtimua aliyekua kocha wake mkuu Joseph Omog na msaidizi wake Ibrahim Shikanda kutokana na timu hiyo kutolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika na timu ya El Merrekh ya Sudan na timu kubaki chini ya kocha raia wa Uganda George Best Nsimbe.

Taarifa ya kitambi kuwa kocha msaidizi wa Azam fc imetolewa kupitia page ya facebook ya timu hiyo.


0 comments:

Post a Comment