Main Menu

Tuesday, February 24, 2015

KOMBE LA DUNIA MWAKA 2022 QATAR KUFANYIKA MWEZI WA KUMI NA MOJA



Hatimaye Kikosi kazi cha Shirikisho la soka Duniani FIFA kilichopewa jukumu la kuchunguza ni muda gani mzuri wa kufanyika kwa fainali za kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022 kimemaliza kazi yake.

Kikosi hicho kinachoongozwa na Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa kimependekeza fainali za kombe la dunia nchini Qatar zifanyike kuanzia mwezi wa kumi na moja na mwezi wa kumi na mbili.

Taarifa zaidi za kikosi kazi hicho zimesema kuwa kipindi cha miezi ya Novemba na Decemba joto hupungua toka nyuzi joto 40 mpaka nyuzi joto 20 mpaka 29.

Taarifa hii imeonekana kupingwa na watu mbalimbali hasa klabu za Ulaya ambazo zinahofia ratiba hiyo ya kombe la dunia inaweza kuingiliana na ratiba ya Ligi za Ulaya.
 
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya England Trevor Sinclair anaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa nchi zilizoshindana na  Qatar kuomba kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022 ambazo ni Australia, Japan, Korea Kusini na Marekani zipewe uenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka huo.

Mchakato wa kumtafuta mwenyeji wa fainali za kombe la dunia umekuwa na malalamiko mengi sana kwani  mchakato huo umehusishwa na rushwa kwa Shirikisho la soka duniani FIFA ambapo Mwaka jana Rais wa FIFA Sepp Blatter aliunda kamati ya kuchunguza mchakato huo kamati iliyoongozwa na mwanasheria Michael Garcia. 

Hata hivyo Ripoti ya Garcia ilionesha kuwa mchakato wa kumpata mwenyeji wa fainali za mwaka 2022 ulikuwa na dosari ripoti ambayo ilipingwa na FIFA wenyewe.

0 comments:

Post a Comment