Main Menu

Wednesday, August 13, 2014

VICENT COMPANY AJITIA KITANZI MANCHESTER CITY

Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany amesaini Mkataba mpya wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
 
Habari za Kompany kupewa Mkataba mpya ambao inaaminika utamfanya sasa awe analipwa Pauni 130,000 kwa wiki, zinakuja saa 24 baada ya kiungo David Silva pia kusaini Mkataba mpya utakaomuweka katika klabu hiyo mwaka 2019.
 
Beki huyo kivutio wa Ubelgiji, ameiongoza Man City kutwa ubingwa wa Ligi Kuu ya England mara mbili katika miaka mitatu iliyopita, pamoja na mataji ya FA na Capital One Cup. Na Kompany, mwenye umri wa miaka 28, anataka kushinda mataji mengine matatu kabla ya kuondoka Etihad.

0 comments:

Post a Comment