Main Menu

Wednesday, February 19, 2014

WAPENDA TATTOO KUWENI MAKINI NA WACHORAJI SEHEMU MSIZOZIONA

 
Haya mambo ya kuchora tattoo hasa katika maeneo ambayo hujioni yana matatizo yake hasa ukikutana na mchoraji asiye muaminifu kwa wateja wake,hebu shuka nayo hii utajua kwanini ni majanga.

Mwanaume aliyedhani amekwenda kwa mchoraji kuchora tattoo ya Dragon mgongoni mwake lakini akajikuta akichorwa kipepeo chenye mfano wa uume(sehemu za siri za mwanaume).

Jambo hilo ambalo limetokea nchini Australia,imewagharimu mchora tattoo na msaidizi wake kwa kuishia jela.

Siku ya Ijumaa Christopher William Lord, 23,alihukumiwa kwenye mahakama ya wilaya ya Ipswich akituhumiwa kwa shambulio la mwili na amehukumiwa kwenda jela miezi 12.

Imeelezwa kuwa mwanaume huyo aliyetaka kuchorwa alikuwa na Brady na Lord wakipata kinywaji na wakamshawishi kumchora tattoo ya Ying Yang ambayo ni alama ya utamaduni wa China na ile ya Dragon.

Lakini walipoingia mkwenye chumba cha kuchorea tattoo,Brady akatengeneza kitu tofauti na walichokubaliana na akachora kipepeo mfano wa uume pia wenye kuonesha kuwa mwanaume huyo ni shoga.

Mteja huyo aliyetaka kuchorwa tattoo alipokuwa akilalamika maumivu na kumtaka Brady kuacha kumchora bado Lord akaendelea kusisitiza atulie maana tattoo inaonekana nzuri na kumuhakikishia kuwa Brady ameanza kuchora tattoo ya dragon baada ya kumaliza ile ya ying yang.

Wakati walipomaliza kuchora tattoo hiyo , Lord akamwambia mteja wake kuwa amemaliza na alipokwenda kuwaonesha marafiki zake tattoo hiyo wakamwambia kuwa amechorwa uume.

Kwa mujibu wa konstebo wa Polisi Paul Malcolm amesema mteja huyo aliambiwa tattoo ni nzuri na haitakiwi kupigwa na jua na asimuoneshe mtu yeyote kwa muda wa wiki moja lakini aliporudi nyumbani akawaonesha watu anaoishi nao na wakamwambia ukweli wa tattoo hiyo.


kwa hisani ya mamaa afrikablog

0 comments:

Post a Comment